Tumezindua rasmi kampeni ya TWENZETU MTANDAONI

Leo tarehe 1 Februari sisi LUMIC BRAND LIMITED tunazindua rasmi kampeni itakayofahamika kama TWENZETU MTANDAONI.

Ni kampeni maalum inayolenga kuwasaidia wajasiriamali, wafanyabiashara, makampuni pamoja na taasisi mbali mbali kufikia wengi na kuongeza mauzo.

Kampeni hii itadumu kwa muda wa miezi mitatu, kuanzia mwezi huu wa pili, mwezi wa tatu na mwezi wa nne, Hivyo mwisho wa kampeni hii ni tarehe 30 Aprili 2024.

Katika kampeni hii tumelenga kuwapa watu majibu kwenye maeneo manne kama ifuatavyo;-

  1. Website solutions
  2. Social media solutions
  3. Graphics Solutions
  4. Corporate production solutions

Kumbuka, wakati wote wa kampeni, kutakuwa na punguzo kubwa la bei, pia kutakuwa na ofa ofa mbalimbali ( mfano; baadhi ya huduma tutazitoa bure kabisa) na bila kusahau tutakuwa tunatoa elimu ya namna bora ya kuwafikia wengi. Endelea kutufuatilia na Twenzetuni Mtandanoni.

#FikiaWengi #TwenzetuMtandaoni

LEAVE A COMMENT